Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
2 Samueli 22:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami. Biblia Habari Njema - BHND Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alinileta, akaniweka mahali pa usalama, alinisalimisha, kwani alipendezwa nami. Neno: Bibilia Takatifu Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. Neno: Maandiko Matakatifu Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. BIBLIA KISWAHILI Akanitoa akanipeleka panapo nafasi; Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. |
Akaondoka huko akachimba kisima kingine, wala hicho hawakukigombania. Akakiita jina lake Rehobothi, akasema, Kwa kuwa sasa BWANA ametufanyia nafasi, nasi tutazidi katika nchi.
lakini akisema kama hivi, Mimi si radhi nawe kabisa; basi, mimi hapa, na anitendee kama aonavyo kuwa vyema.
Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Kwa maana Israeli ametenda kwa ukaidi, kama ndama mkaidi; sasa je! BWANA atawalisha kama mwana-kondoo katika mahali penye malisho mazuri.
Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.