Naye akapita kati ya kabila zote za Israeli mpaka Abeli, na kwa Bethmaaka na Wabikri wote; nao wakakusanyika, wakaenda pia kumwandama.
2 Samueli 20:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini. Biblia Habari Njema - BHND Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakaenda kumzingira Sheba akiwa katika mji huo wa Abeli wa Beth-maaka. Walirundika kuuzingira mji, na ngome; halafu wakaanza kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini. Neno: Bibilia Takatifu Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumzingira Sheba mwana wa Bikri huko Abel-Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya mji. Walipokuwa wakijaribu kuubomoa ukuta ili kuuangusha chini, Neno: Maandiko Matakatifu Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumhusuru Sheba mwana wa Bikri huko Abel-Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya mji. Walipokuwa wanagongagonga ukuta ili kuubomoa na kuuangusha chini, BIBLIA KISWAHILI Na hao wakaja wakauzingira katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya kilima mbele ya mji, nacho kikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunjavunja ukuta, wapate kuubomoa. |
Naye akapita kati ya kabila zote za Israeli mpaka Abeli, na kwa Bethmaaka na Wabikri wote; nao wakakusanyika, wakaenda pia kumwandama.
Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.
Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.
Basi BWANA asema hivi katika habari za mfalme wa Ashuru, Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
Palikuwa na mji mdogo, uliokuwa na watu wachache ndani yake; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga.
Basi, BWANA asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru, Yeye hataingia ndani ya mji huu, wala hatapiga mshale hapa, wala hatakuja mbele yake kwa ngao, wala hatajenga boma juu yake.
angalia maboma haya; wameujia mji huu ili kuutwaa; na mji huu umetiwa katika mikono ya Wakaldayo wanaopigana nao, kwa sababu ya upanga, na njaa, na tauni; na hayo uliyosema yamekuwa; na, tazama, wewe unayaona.
Maana BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi, kuhusu nyumba za mji huu, na kuhusu nyumba za wafalme wa Yuda, zilizobomolewa ili kuyapinga maboma na upanga;
Maana BWANA wa majeshi asema hivi, Jikatieni miti, mjenge boma juu ya Yerusalemu. Mji huu ni mji unaojiwa; dhuluma tupu imo ndani yake.
ukauhusuru, ukajenge ngome juu yake, na kufanya boma juu yake; ukaweke makambi juu yake, na kuweka magogo ya kuubomoa yauzunguke pande zote.
Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;