Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
2 Samueli 16:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa ushauri wako, tufanyeje. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Absalomu alipomwambia Ahithofeli, “Nishauri; tufanye nini?” Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Absalomu alipomwambia Ahithofeli, “Nishauri; tufanye nini?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Absalomu alipomwambia Ahithofeli, “Nishauri; tufanye nini?” Neno: Bibilia Takatifu Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe ushauri wako. Tufanye nini?” Neno: Maandiko Matakatifu Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako. Tufanye nini?” BIBLIA KISWAHILI Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, Haya, toa ushauri wako, tufanyeje. |
Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Na tena, Ni nani ambaye yanipasa nimtumikie? Hainipasi kumtumikia mwanawe? Kama nilivyomtumikia baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mbele yako.
Naye Ahithofeli akamwambia Absalomu, Ingia wewe kwa masuria wa baba yako, hao aliowaacha ili kutunza nyumba; na Israeli wote watasikia ya kuwa umechukizwa kabisa na baba yako; ndipo itatiwa nguvu mikono yao wote walio pamoja nawe.
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;