Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Samueli 14:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, Absalomu akawaambia watumishi wake, “Angalieni Yoabu ana shamba la shayiri karibu na langu. Nendeni mkalichome moto.” Kwa hiyo watumishi wa Absalomu wakalichoma moto shamba la Yoabu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, Absalomu akawaambia watumishi wake, “Angalieni Yoabu ana shamba la shayiri karibu na langu. Nendeni mkalichome moto.” Kwa hiyo watumishi wa Absalomu wakalichoma moto shamba la Yoabu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, Absalomu akawaambia watumishi wake, “Angalieni Yoabu ana shamba la shayiri karibu na langu. Nendeni mkalichome moto.” Kwa hiyo watumishi wa Absalomu wakalichoma moto shamba la Yoabu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ndipo akawaambia watumishi wake, “Tazama, shamba la Yoabu liko jirani na langu, naye ana shayiri humo. Nendeni mkaitie moto.” Kisha watumishi wa Absalomu wakalitia moto shamba hilo.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ndipo akawaambia watumishi wake, “Tazama, shamba la Yoabu liko jirani na langu, naye ana shayiri humo. Nendeni mkalitie moto.” Kisha watumishi wa Absalomu wakalitia moto shamba hilo.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Samueli 14:30
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Absalomu akatuma Yoabu aitwe, amtume kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja.

Ndipo akaondoka Yoabu, akamwendea Absalomu nyumbani kwake, akamwambia, Kwa nini watumishi wako wamelitia moto shamba langu?

Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua mikuki mitatu midogo mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa bado hai katikati ya ule mwaloni.

Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyagakanyaga.

Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia kwa hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru.