2 Petro 1:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Biblia Habari Njema - BHND uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza uchaji wenu kwa urafiki wa kindugu, na urafiki wenu wa kindugu kwa mapendo. Neno: Bibilia Takatifu katika utauwa, upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu, upendo. Neno: Maandiko Matakatifu katika utauwa, upendano wa ndugu; na katika upendano wa ndugu, upendo. BIBLIA KISWAHILI na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. |
Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;
Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.
Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.