Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




2 Mambo ya Nyakati 9:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, kwa wingi kila mwaka.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kila mmoja wao alimletea zawadi: Vyombo vya fedha na vya dhahabu, mavazi na silaha manukato, farasi na nyumbu. Zawadi hizi alizipokea kila mwaka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kila mmoja wao alimletea zawadi: Vyombo vya fedha na vya dhahabu, mavazi na silaha manukato, farasi na nyumbu. Zawadi hizi alizipokea kila mwaka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kila mmoja wao alimletea zawadi: vyombo vya fedha na vya dhahabu, mavazi na silaha manukato, farasi na nyumbu. Zawadi hizi alizipokea kila mwaka.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezo, farasi na nyumbu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mwaka baada ya mwaka, kila mmoja ambaye alikuja, alileta zawadi, vyombo vya fedha na dhahabu, majoho, silaha na vikolezi, farasi na nyumbu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, kwa wingi kila mwaka.

Tazama sura
Tafsiri zingine



2 Mambo ya Nyakati 9:24
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi akampa mfalme talanta za dhahabu mia moja na ishirini, na manukato mengi, mengi sana, na vito vya thamani; wala haukuja tena wingi wa manukato, kama hayo malkia wa Sheba aliyompa mfalme Sulemani.


Wakaleta kila mtu zawadi yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, na silaha, na manukato, na farasi, na nyumbu, hesabu yake ya mwaka kwa mwaka.


Hiramu alikuwa amemletea mfalme talanta mia moja na ishirini za dhahabu.


Na baadhi ya Wafilisti walimletea Yehoshafati zawadi, na fedha ya kodi; Waarabu nao wakamletea kondoo dume elfu saba na mia saba, na mabeberu elfu saba na mia saba.


Wafalme wote wa duniani wakamtafuta Sulemani uso wake, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.


Basi akampa mfalme talanta mia moja na ishirini za dhahabu, na manukato mengi mengi sana, na vito vya thamani; wala hapakuwapo manukato mengi kama hayo aliyopewa mfalme Sulemani na malkia wa Sheba.


Ndipo wakamwendea ndugu zake wote, wanaume kwa wanawake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakampa pole na kumliwaza kwa ajili ya mateso hayo yote aliyoleta BWANA juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja.


Mkemee mnyama wa mafunjoni; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita.


Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.


Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.


Lakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.