basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
2 Mambo ya Nyakati 9:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno alilofichiwa Sulemani, asimwambie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza. Biblia Habari Njema - BHND Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Solomoni aliyajibu maswali yote; hapakuwapo na jambo lolote aliloshindwa kumweleza. Neno: Bibilia Takatifu Sulemani alimjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake hata asiweze kumwelezea. Neno: Maandiko Matakatifu Sulemani akamjibu maswali yake yote, wala hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwake asiweze kumwelezea. BIBLIA KISWAHILI Naye Sulemani akamfumbulia maswali yake yote; wala halikuwako neno aliloficha Sulemani, asimwambie. |
basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.
Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
Na malkia wa Sheba aliposikia sifa za Sulemani, alikuja ili amjaribu Sulemani kwa maswali ya fumbo huko Yerusalemu, akiwa na wafuasi wengi, na ngamia wachukuao manukato, na dhahabu nyingi sana, na vito vya thamani; alipomfikia Sulemani, akamwambia mambo yote aliyokuwa nayo moyoni mwake.
Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi; Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje, yote hufanywa kwa mifano,
wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.