Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.
2 Mambo ya Nyakati 8:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya BWANA, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi miradi yote ya Solomoni aliyofanya tangu jiwe la msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu lilipowekwa ilikamilika. Hivyo nyumba ya Mwenyezi-Mungu ilimalizika. Biblia Habari Njema - BHND Basi miradi yote ya Solomoni aliyofanya tangu jiwe la msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu lilipowekwa ilikamilika. Hivyo nyumba ya Mwenyezi-Mungu ilimalizika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi miradi yote ya Solomoni aliyofanya tangu jiwe la msingi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu lilipowekwa ilikamilika. Hivyo nyumba ya Mwenyezi-Mungu ilimalizika. Neno: Bibilia Takatifu Kazi yote ya Mfalme Sulemani ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu ulipowekwa hadi kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la Mwenyezi Mungu likamalizika kujengwa. Neno: Maandiko Matakatifu Kazi yote ya Mfalme Sulemani ilifanyika kuanzia siku msingi wa Hekalu la bwana ulipowekwa mpaka kukamilika kwake. Kwa hiyo Hekalu la bwana likamalizika kujengwa. BIBLIA KISWAHILI Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya BWANA, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya BWANA. |
Na waashi wa Sulemani na waashi wa Hiramu na Wagebali wakayachonga, wakaweka tayari miti na mawe ya kuijenga nyumba.
Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.
Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lolote, wala kwa habari ya hazina.