Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji la pili.
2 Mambo ya Nyakati 4:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema pia mifano ya makomamanga 400 kwa ajili ya nyavu hizo mbili, safu mbilimbili za makomamanga kwa kila wavu, ili kupamba mabakuli yale mawili ya taji zilizokuwa juu ya kila nguzo. Biblia Habari Njema - BHND pia mifano ya makomamanga 400 kwa ajili ya nyavu hizo mbili, safu mbilimbili za makomamanga kwa kila wavu, ili kupamba mabakuli yale mawili ya taji zilizokuwa juu ya kila nguzo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza pia mifano ya makomamanga 400 kwa ajili ya nyavu hizo mbili, safu mbilimbili za makomamanga kwa kila wavu, ili kupamba mabakuli yale mawili ya taji zilizokuwa juu ya kila nguzo. Neno: Bibilia Takatifu yale makomamanga mia nne kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo); Neno: Maandiko Matakatifu yale makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo); BIBLIA KISWAHILI na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo. |
Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji la pili.
Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kulia, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto, akaiita jina lake Boazi.
zile nguzo mbili, na mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo; na nyavu mbili za kuvifunika hivyo viumbe viwili vya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;
na makomamanga mia nne ya zile nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika nayo mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;
Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia moja, akayaweka juu ya hiyo minyororo.
zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;
Palikuwa na makomamanga tisini na sita katika pande zake; makomamanga; yote yalikuwa mia moja juu ya wavu huo pande zote.