2 Mambo ya Nyakati 4:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huramu alitengeneza vyungu, sepetu na mabirika. Basi Huramu akamaliza kazi aliyomfanyia mfalme Solomoni kuhusu nyumba ya Mungu: Biblia Habari Njema - BHND Huramu alitengeneza vyungu, sepetu na mabirika. Basi Huramu akamaliza kazi aliyomfanyia mfalme Solomoni kuhusu nyumba ya Mungu: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huramu alitengeneza vyungu, sepetu na mabirika. Basi Huramu akamaliza kazi aliyomfanyia mfalme Solomoni kuhusu nyumba ya Mungu: Neno: Bibilia Takatifu Huramu pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza: Neno: Maandiko Matakatifu Pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza, yaani: BIBLIA KISWAHILI Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni. Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; |
Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.
Tena toka Tibhathi, na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno, aliyoitumia Sulemani katika kutengeneza lile birika la shaba, na zile nguzo, na vile vyombo vya shaba.
zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;