Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.
2 Mambo ya Nyakati 36:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake; wala hakujinyenyekeza mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, wala hakunyenyekea mbele ya nabii Yeremia ambaye alisema maneno yaliyotoka kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, wala hakunyenyekea mbele ya nabii Yeremia ambaye alisema maneno yaliyotoka kwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, wala hakunyenyekea mbele ya nabii Yeremia ambaye alisema maneno yaliyotoka kwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Alifanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Alifanya maovu machoni pa bwana Mwenyezi Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la bwana. BIBLIA KISWAHILI akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake; wala hakujinyenyekeza mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha BWANA. |
Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.
Hata alipokuwa katika taabu, akamsihi BWANA, Mungu wake, akajinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.
Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika Kumbukumbu ya Hozai.
Wala hakujinyenyekeza mbele za BWANA, kama Manase babaye alivyojinyenyekeza; lakini huyo Amoni akaongeza makosa juu ya makosa.
Lakini Yosia hakukubali kumwachia, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.
Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.
Maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani waliokuwa katika Anathothi, katika nchi ya Benyamini;
Nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa mfano wa maneno hayo yote, nikisema, Tieni shingo zenu katika nira ya mfalme wa Babeli, mkamtumikie yeye na watu wake, mpate kuishi.