2 Mambo ya Nyakati 33:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye BWANA akasema na Manase, na watu wake; wala wasiangalie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alimwonya Manase na watu wake, lakini hawakumsikia. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alimwonya Manase na watu wake, lakini hawakumsikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alimwonya Manase na watu wake, lakini hawakumsikia. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. Neno: Maandiko Matakatifu bwana akasema na Manase pamoja na watu wake, lakini hawakumjali. BIBLIA KISWAHILI Naye BWANA akasema na Manase, na watu wake; wala wasiangalie. |
Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji walionena naye kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa kati ya mambo ya wafalme wa Israeli.
Basi Manase aliwapotosha Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, hata wakazidi kufanya mabaya kuliko mataifa, aliowaharibu BWANA mbele ya wana wa Israeli.
Msiwe ninyi kama baba zenu, ambao manabii wa zamani waliwalilia, wakisema, BWANA wa majeshi asema hivi, Rudini sasa, na kuziacha njia zenu mbovu, na matendo yenu maovu; lakini hawakusikia, wala kunitii, asema BWANA.