Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.
2 Mambo ya Nyakati 30:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa furaha kuu katika Yerusalemu; kwa sababu tangu siku za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hayajakuwako mambo kama hayo huko Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kukawa na furaha kuu mno Yerusalemu, maana tangu enzi ya mfalme Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, jambo kama hilo lilikuwa halijatokea Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND Kukawa na furaha kuu mno Yerusalemu, maana tangu enzi ya mfalme Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, jambo kama hilo lilikuwa halijatokea Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kukawa na furaha kuu mno Yerusalemu, maana tangu enzi ya mfalme Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, jambo kama hilo lilikuwa halijatokea Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Kulikuwa na furaha kubwa katika Yerusalemu, kwa sababu tangu siku za Mfalme Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli halijakuwepo jambo kama hili huko Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Kulikuwa na furaha kubwa katika Yerusalemu, kwa sababu tangu siku za Mfalme Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli halijakuwepo jambo kama hili katika Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Ikawa furaha kuu katika Yerusalemu; kwa sababu tangu siku za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hayajakuwako mambo kama hayo huko Yerusalemu. |
Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie BWANA sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainamisha vichwa, wakaabudu.
Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
Wala haikufanyika Pasaka kama ile katika Israeli tangu siku za nabii Samweli; wala wafalme wa Israeli hawakufanya hata mmoja wao Pasaka kama ile Yosia aliyoifanya, pamoja na makuhani, na Walawi, na Yuda wote na Israeli waliokuwapo, na wenyeji wa Yerusalemu.
Na mkutano wote wa watu, waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, wakatengeneza vibanda, wakakaa katika vibanda hivyo; maana tangu siku za Yoshua, mwana wa Nuni, hadi siku ile, wana wa Israeli hawakufanya hivyo. Pakawa na furaha kubwa sana.