Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
2 Mambo ya Nyakati 30:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, BWANA, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema atakayekuomba kwa moyo wake wote wewe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hata ingawa si msafi kulingana na sheria za utakaso.” Biblia Habari Njema - BHND atakayekuomba kwa moyo wake wote wewe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hata ingawa si msafi kulingana na sheria za utakaso.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza atakayekuomba kwa moyo wake wote wewe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hata ingawa si msafi kulingana na sheria za utakaso.” Neno: Bibilia Takatifu ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake, hata kama yeye si safi kulingana na sheria za mahali patakatifu.” Neno: Maandiko Matakatifu ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, bwana, Mungu wa baba zake, hata kama yeye si safi kulingana na sheria za mahali patakatifu.” BIBLIA KISWAHILI aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, BWANA, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu. |
Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Ee BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, baba zetu, ulidumishe jambo hili milele katika fikira za mawazo ya mioyo ya watu wako, ukaiongoze mioyo yao kwako;
Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.
Lakini mahali pa juu hapakuondolewa; wala mioyo ya watu bado haijakazwa kwa Mungu wa baba zao.
Wana wa Israeli wakaila, wale waliorudi kutoka nchi ya uhamisho wao, na watu wote ambao pamoja nao wamejitenga na uchafu wa taifa za nchi, ili kumtaka BWANA, Mungu wa Israeli,
Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.
Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamwelekezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.