Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa, wakaingia, kama alivyoamuru mfalme kwa maneno ya BWANA, ili waisafishe nyumba ya BWANA.
2 Mambo ya Nyakati 30:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku ya kumi na nne ya mwezi huo walichinja mwanakondoo wa Pasaka. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketeza katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Siku ya kumi na nne ya mwezi huo walichinja mwanakondoo wa Pasaka. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketeza katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku ya kumi na nne ya mwezi huo walichinja mwanakondoo wa Pasaka. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketeza katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kisha wakamchinja mwana-kondoo wa Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketezwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha wakamchinja mwana-kondoo wa Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketezwa katika Hekalu la bwana. BIBLIA KISWAHILI Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA. |
Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa, wakaingia, kama alivyoamuru mfalme kwa maneno ya BWANA, ili waisafishe nyumba ya BWANA.
Na hesabu ya sadaka hizo za kuteketezwa mkutano walizozileta ni ng'ombe dume sabini, kondoo dume mia moja, na wana-kondoo mia mbili; hao wote walikuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Lakini makuhani walikuwa wachache, wasiweze kuchuna sadaka zote za kuteketezwa; basi ndugu zao Walawi wakawasaidia, hadi kazi ilipokwisha na hadi makuhani walipojitakasa; kwa kuwa Walawi walikuwa wenye mioyo ya adili kwa kujitakasa kuliko makuhani.
Basi watu wengi wakakusanyika Yerusalemu watu wengi ili kuifanya sikukuu ya mikate isiyochachwa katika mwezi wa pili, kusanyiko kuu sana.
Kwa maana mfalme na wakuu wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikubaliana kuiadhimisha Pasaka mwezi wa pili.
Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.
Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani wa kutosha walikuwa hawajajitakasa, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.
na wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wadogo wao wote, wake zao, na wana wao, na binti zao, katika kusanyiko lote; kwani kwa vile walivyoaminiwa, wakajitakasa katika utakatifu;
Mkachinje Pasaka, mkajitakase, mkawatengenezee ndugu zenu, kutenda sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Musa.
Ikawa makuhani walipokwisha kutoka katika patakatifu; (kwani makuhani wote waliokuwapo, walikuwa wamejitakasa, wala hawakuzishika zamu zao;
Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja Pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao.
BWANA akamwambia Musa, Nenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao,
mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;