Hakika yake haikufanyika Pasaka kama hiyo, tangu zamani za waamuzi waliowaamua Israeli, wala katika zamani za wafalme wa Israeli, wala za wafalme wa Yuda.
2 Mambo ya Nyakati 30:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi watu wengi wakakusanyika Yerusalemu watu wengi ili kuifanya sikukuu ya mikate isiyochachwa katika mwezi wa pili, kusanyiko kuu sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wengi sana walijumuika mjini Yerusalemu mnamo mwezi wa pili, kuiadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. Biblia Habari Njema - BHND Watu wengi sana walijumuika mjini Yerusalemu mnamo mwezi wa pili, kuiadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wengi sana walijumuika mjini Yerusalemu mnamo mwezi wa pili, kuiadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. Neno: Bibilia Takatifu Basi umati mkubwa wa watu wakakusanyika huko Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu katika mwezi wa pili. Neno: Maandiko Matakatifu Basi umati mkubwa wa watu ukakusanyika huko Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu katika mwezi wa pili. BIBLIA KISWAHILI Basi watu wengi wakakusanyika Yerusalemu watu wengi ili kuifanya sikukuu ya mikate isiyochachwa katika mwezi wa pili, kusanyiko kuu sana. |
Hakika yake haikufanyika Pasaka kama hiyo, tangu zamani za waamuzi waliowaamua Israeli, wala katika zamani za wafalme wa Israeli, wala za wafalme wa Yuda.
Wakainuka, wakaziondoa madhabahu zilizokuwamo Yerusalemu, nazo madhabahu za kufukizia wakaziondoa, wakazitupa katika kijito Kidroni.
Kisha wakaichinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa BWANA.
Kwa maana mfalme na wakuu wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikubaliana kuiadhimisha Pasaka mwezi wa pili.
Naye Yosia akamfanyia BWANA Pasaka huko Yerusalemu; wakachinja Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, yeyote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA;