Yakaenea mabawa ya makerubi hayo dhiraa ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba.
2 Mambo ya Nyakati 3:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akalifanya pazia la samawati na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaitengeneza makerubi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitengeneza pazia kwa kitambaa cha kitani safi, cha rangi ya samawati, ya zambarau na nyekundu. Alilinakshi kwa michoro ya viumbe wenye mabawa. Biblia Habari Njema - BHND Alitengeneza pazia kwa kitambaa cha kitani safi, cha rangi ya samawati, ya zambarau na nyekundu. Alilinakshi kwa michoro ya viumbe wenye mabawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitengeneza pazia kwa kitambaa cha kitani safi, cha rangi ya samawati, ya zambarau na nyekundu. Alilinakshi kwa michoro ya viumbe wenye mabawa. Neno: Bibilia Takatifu Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake. Neno: Maandiko Matakatifu Akatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na za kitani safi, na kutarizi makerubi juu yake. BIBLIA KISWAHILI Akalifanya pazia la samawati na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaitengenezea makerubi. |
Yakaenea mabawa ya makerubi hayo dhiraa ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba.
Na hilo pazia la lango la ua, lilikuwa ni kazi ya mwenye kutia taraza, lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri ya kusokotwa; lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini, na kutukuka kwake katika huo upana wake kulikuwa dhiraa tano, kupatana na ile chandarua ya ua.
hapo watakapoanza safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha pazia la sitara, na kulifunika sanduku la ushahidi kwa hilo pazia;
Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;