Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.
2 Mambo ya Nyakati 29:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama aliyoyafanya Daudi babaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama vile alivyofanya Daudi, babu yake. Biblia Habari Njema - BHND Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama vile alivyofanya Daudi, babu yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitenda mema mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama vile alivyofanya Daudi, babu yake. Neno: Bibilia Takatifu Akafanya yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu kama Daudi baba yake alivyofanya. Neno: Maandiko Matakatifu Akafanya yaliyo mema machoni pa bwana kama Daudi baba yake alivyofanya. BIBLIA KISWAHILI Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama aliyoyafanya Daudi babaye. |
Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.
Naye BWANA alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute Mabaali;
lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli.
Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama Daudi babaye;
Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaziendea njia za Daudi babaye, asigeuke kwa kulia wala kwa kushoto.