Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamejisababishia machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakatuma talanta elfu moja za fedha ili kukodi magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
2 Mambo ya Nyakati 25:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaajiri pia watu mashujaa elfu mia moja wa Israeli kwa talanta mia moja za fedha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha. Biblia Habari Njema - BHND Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena, alikodisha askari wengine mashujaa 1,000 kutoka Israeli, kwa gharama ya kilo 3,000 za fedha. Neno: Bibilia Takatifu Akawaajiri pia wapiganaji elfu mia moja kutoka Israeli kwa talanta mia moja za fedha. Neno: Maandiko Matakatifu Akawaajiri pia watu 100,000 wapiganaji kutoka Israeli kwa talanta 100 za fedha. BIBLIA KISWAHILI Akaajiri pia watu mashujaa elfu mia moja wa Israeli kwa talanta mia moja za fedha. |
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamejisababishia machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakatuma talanta elfu moja za fedha ili kukodi magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.
Lakini mtu wa Mungu akamjia, akasema, Ee mfalme, usiwaruhusu jeshi la Israeli waende nawe; kwa kuwa BWANA hayupo pamoja na Israeli, yaani, wana wote wa Efraimu.