Walakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
2 Mambo ya Nyakati 25:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, lakini si kwa moyo mkamilifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu ingawa hakuyatenda kwa moyo mnyofu. Biblia Habari Njema - BHND Alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu ingawa hakuyatenda kwa moyo mnyofu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alitenda yaliyo mema mbele ya Mwenyezi-Mungu ingawa hakuyatenda kwa moyo mnyofu. Neno: Bibilia Takatifu Akatenda yaliyo mema machoni pa Mwenyezi Mungu, lakini sio kwa moyo wake wote. Neno: Maandiko Matakatifu Akatenda yaliyo mema machoni pa bwana, lakini sio kwa moyo wake wote. BIBLIA KISWAHILI Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, lakini si kwa moyo mkamilifu. |
Walakini mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.
Basi ikawa, Amazia alipokwisha rudi kutoka kuwaua Waedomi, alileta miungu ya wana wa Seiri, akaisimamisha kuwa miungu yake, akaisujudia, akaifukizia uvumba.
Basi ikawa, alipojiimarisha katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye.
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Moyo wao umegawanyika; sasa wataonekana kuwa na hatia; yeye atazipiga madhabahu zao, ataziharibu nguzo zao.
Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.