Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




2 Mambo ya Nyakati 25:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wakiwa hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha chini toka juu ya jabali, hadi wakavunjikavunjika wote.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Waliteka watu 10,000, wakawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini miambani, wakapondeka vipandevipande.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Waliteka watu 10,000, wakawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini miambani, wakapondeka vipandevipande.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Waliteka watu 10,000, wakawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini miambani, wakapondeka vipandevipande.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Jeshi la Yuda pia likawateka watu elfu kumi wakiwa hai, likawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini kwa nguvu, wote wakavunjika vipande vipande.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Jeshi la Yuda pia likawateka watu 10,000 wakiwa hai, likawapandisha juu ya jabali na kuwatupa chini kwa nguvu hata wote wakavunjika vipande vipande.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wakiwa hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha chini toka juu ya jabali, hadi wakavunjikavunjika wote.

Tazama sura
Tafsiri zingine



2 Mambo ya Nyakati 25:12
8 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.


Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawawafanyisha kazi kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.


Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;


Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi, akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi.


Lakini wanajeshi, aliowarudisha Amazia, wasiende naye vitani, hao wakaiteka miji ya Yuda, tangu Samaria mpaka Beth-horoni, wakawapiga watu elfu tatu, wakachukua nyara nyingi.


Kwa hiyo hasira ya BWANA ikawaka juu ya Amazia, akamtuma kwake nabii, aliyemwambia, Mbona umeitafuta miungu ya watu, isiyowaokoa watu wao mkononi mwako?


Wakuu wao wakiangushwa kando ya genge, Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.