Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Mambo ya Nyakati 25:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ndipo Amazia akaachilia jeshi lililomjia kutoka Efraimu, ili warudi kwao; kwa hiyo hasira yao ikawaka sana juu ya Yuda, nao wakarudi kwao wenye hasira kali.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hapo Amazia akawaachia wanajeshi waliotoka Efraimu warudi makwao. Basi wakarejea kwao wakiwa wamewakasirikia sana watu wa Yuda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hapo Amazia akawaachia wanajeshi waliotoka Efraimu warudi makwao. Basi wakarejea kwao wakiwa wamewakasirikia sana watu wa Yuda.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hapo Amazia akawaachia wanajeshi waliotoka Efraimu warudi makwao. Basi wakarejea kwao wakiwa wamewakasirikia sana watu wa Yuda.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hivyo Amazia akayaondoa yale majeshi yaliyokuwa yamekuja kutoka Efraimu na kuyarudisha nyumbani. Waliwakasirikia sana Yuda, nao wakarudi nyumbani wakiwa na hasira kali.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hivyo Amazia akayaondoa yale majeshi yaliyokuwa yamekuja kutoka Efraimu na kuyarudisha nyumbani. Waliwakasirikia sana Yuda, nao wakarudi nyumbani wakiwa na hasira kali.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ndipo Amazia akaachilia jeshi lililomjia kutoka Efraimu, ili warudi kwao; kwa hiyo hasira yao ikawaka sana juu ya Yuda, nao wakarudi kwao wenye hasira kali.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Mambo ya Nyakati 25:10
5 Marejeleo ya Msalaba  

Hao watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, wakasema, Sisi tunazo sehemu kumi katika mfalme, tena tunayo haki yetu katika Daudi zaidi kuliko ninyi; mbona basi ninyi mmetudharau sisi, msitake ushauri wetu kwanza katika kumrudisha tena mfalme wetu? Na maneno ya watu wa Yuda yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.

BWANA asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la BWANA, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la BWANA.

Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi, akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi.

Amazia akamwambia mtu wa Mungu, Lakini tuzifanyieje zile talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, BWANA aweza kukupa zaidi sana kuliko hizo.

Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.