Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
2 Mambo ya Nyakati 24:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na hawa ndio waliomfanyia fitina, Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu waliomfanyia njama walikuwa Zabadi mwana wa mwanamke Mwamoni jina lake Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa mwanamke Mmoabu jina lake Shimrithi. Biblia Habari Njema - BHND Watu waliomfanyia njama walikuwa Zabadi mwana wa mwanamke Mwamoni jina lake Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa mwanamke Mmoabu jina lake Shimrithi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu waliomfanyia njama walikuwa Zabadi mwana wa mwanamke Mwamoni jina lake Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa mwanamke Mmoabu jina lake Shimrithi. Neno: Bibilia Takatifu Wale waliopanga njama dhidi yake walikuwa Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabu. Neno: Maandiko Matakatifu Wale waliofanya hila mbaya dhidi yake walikuwa Zabadi, mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, Yehozabadi, mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabu. BIBLIA KISWAHILI Na hawa ndio waliomfanyia fitina, Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi. |
Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Basi kwa habari ya wanawe, na ukubwa wa mizigo aliolemewa, na majengo ya nyumba ya Mungu, tazama, hayo yameandikwa katika maelezo ya kitabu cha Wafalme. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake.
Basi ikawa, alipojiimarisha katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye.