Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.
2 Mambo ya Nyakati 24:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme. Biblia Habari Njema - BHND Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadui walipoondoka, walimwacha akiwa amejeruhiwa vibaya sana, maofisa wake wakala njama wakamwulia kitandani mwake, kulipiza kisasi mauaji ya mwana wa kuhani Yehoyada. Alizikwa katika mji wa Daudi, lakini si kwenye makaburi ya wafalme. Neno: Bibilia Takatifu Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuua kitandani mwake. Hivyo akafa, wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme. Neno: Maandiko Matakatifu Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme. BIBLIA KISWAHILI Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme. |
Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.
Akarudi Yezreeli ili aponye majeraha waliyomjeruhi huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu, katika Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Akamtafuta Ahazia, wakamkamata, (naye alikuwa amejificha Samaria,) wakamleta kwa Yehu, wakamwua; wakamzika, kwa maana wakasema, Huyu ni mwana wa Yehoshafati, huyo aliyemtafuta BWANA kwa moyo wake wote. Wala nyumba ya Ahazia hawakuwa na uwezo wa kuushika ufalme.
Wakamzika katika mji wa Daudi kati ya wafalme, kwa sababu ametenda mema katika Israeli, na kwa Mungu, na katika nyumba yake.
Na hawa ndio waliomfanyia fitina, Zabadi mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, na Yehozabadi mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi.
Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.
Basi ikawa, alipojiimarisha katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye.
Ahazi akalala na babaze, wakamzika mjini, yaani, Yerusalemu; maana hawakumleta makaburini mwa wafalme wa Israeli; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.