Mfalme wa Israeli akawaambia watumishi wake, Je! Hamjui ya kuwa Ramoth-Gileadi ni yetu? Nasi tumenyamaza tusiitwae mkononi mwa mfalme wa Shamu?
2 Mambo ya Nyakati 22:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye akaenda kwa mashauri yao, akafuatana na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli ili kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-gileadi; nao Washami wakamjeruhi Yoramu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata alifuata shauri lao, akaenda pamoja na mfalme Yehoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-gileadi. Nao Washamu walimjeruhi Yoramu. Biblia Habari Njema - BHND Hata alifuata shauri lao, akaenda pamoja na mfalme Yehoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-gileadi. Nao Washamu walimjeruhi Yoramu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata alifuata shauri lao, akaenda pamoja na mfalme Yehoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-gileadi. Nao Washamu walimjeruhi Yoramu. Neno: Bibilia Takatifu Pia akafuata ushauri wao alipoenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu. Neno: Maandiko Matakatifu Pia akafuata shauri lao alipokwenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu. BIBLIA KISWAHILI Naye akaenda kwa mashauri yao, akafuatana na Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli ili kupigana na Hazaeli mfalme wa Shamu huko Ramoth-gileadi; nao Washami wakamjeruhi Yoramu. |
Mfalme wa Israeli akawaambia watumishi wake, Je! Hamjui ya kuwa Ramoth-Gileadi ni yetu? Nasi tumenyamaza tusiitwae mkononi mwa mfalme wa Shamu?
Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba.
Basi Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.
Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, za kila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mizigo ya ngamia arubaini, akaenda, akasimama mbele yake akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, amenituma kwako, kusema, Je nitapona ugonjwa huu?
Nabii Elisha akamwita mmojawapo wa wana wa manabii, akamwambia, Jikaze viuno, ukachukue chupa hii ya mafuta mkononi mwako, ukaende Ramoth-Gileadi.
Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Je! Utakwenda nami mpaka Ramoth-gileadi? Akamjibu, Mimi ni kama wewe, na watu wangu kama watu wako; nasi tutakuwa pamoja nawe vitani.
Ikawa makamanda wa magari walipomwona Yehoshafati, wakasema, Mfalme wa Israeli ni huyu. Basi wakamgeukia ili wapigane naye; lakini Yehoshafati akalia, na BWANA akamsaidia; Mungu akawaondoa kwake.
Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.
Akarudi Yezreeli ili aponye majeraha waliyomjeruhi huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu, katika Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.