Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
2 Mambo ya Nyakati 21:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakati wa enzi zake Edomu wakaasi utawala wa Yuda, wakajifanyia mfalme. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati wa enzi ya Yehoramu, watu wa Edomu waliasi utawala wa Yuda, wakamtawaza mfalme wao wenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Wakati wa enzi ya Yehoramu, watu wa Edomu waliasi utawala wa Yuda, wakamtawaza mfalme wao wenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati wa enzi ya Yehoramu, watu wa Edomu waliasi utawala wa Yuda, wakamtawaza mfalme wao wenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Wakati wa utawala wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. BIBLIA KISWAHILI Wakati wa enzi zake Edomu wakaasi utawala wa Yuda, wakajifanyia mfalme. |
Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
Basi mfalme wa Israeli akaenda, na mfalme wa Yuda, na mfalme wa Edomu; wakazunguka mwendo wa siku saba; wala hapakuwa na maji kwa jeshi, wala kwa wanyama waliowafuata.
Hivyo Edomu wakaasi utawala wa Yuda hata leo; wakati huo uo nao Libna wakaasi utawala wake: kwa sababu alikuwa amemwacha BWANA, Mungu wa baba zake.
Ndipo Yehoramu akavuka na makamanda wake, na magari yake yote pamoja naye; akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na hao makamanda wa magari.