Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
2 Mambo ya Nyakati 21:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujiimarisha, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yehoramu alipokikalia kiti cha enzi na utawala wake ulipokuwa umekwisha imarika, yeye aliwaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia baadhi ya wakuu wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Yehoramu alipokikalia kiti cha enzi na utawala wake ulipokuwa umekwisha imarika, yeye aliwaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia baadhi ya wakuu wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yehoramu alipokikalia kiti cha enzi na utawala wake ulipokuwa umekwisha imarika, yeye aliwaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia baadhi ya wakuu wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Yehoramu kujiimarisha katika ufalme wa baba yake, akawaua kwa upanga ndugu zake wote pamoja na baadhi ya wakuu wa Israeli. BIBLIA KISWAHILI Basi Yehoramu alipoinuliwa juu ya ufalme wa babaye, na kujiimarisha, akawaua nduguze wote kwa upanga, na baadhi ya wakuu wa Israeli pia. |
Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
Haya basi, nikupe shauri, tafadhali, upate kuiokoa roho yako, na roho ya mwanao Sulemani.
lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe;
nao wakakwea juu ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekama nyumbani mwa mfalme, na wanawe pia, na wakeze; asibakizwe mtoto hata mmoja, ila Ahazia, aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe.
Basi Athalia, mama wa Ahazia, alipoona ya kuwa mwanawe amekufa, akainuka, akawaangamiza jamaa yote ya kifalme ya nyumba ya Yuda.
Ikawa, Yehu alipokuwa akiwafanyia hukumu nyumba ya Ahabu, aliwakuta wakuu wa Yuda, na wana wa nduguze Ahazia, wakimtumikia Ahazia, akawaua.
Basi ikawa, alipojiimarisha katika ufalme wake, akawaua watumishi wale waliomwua mfalme babaye.
si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze, hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini Yothamu, mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha.