Nao wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake, lililokuwako Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, wakapambazukiwa huko Hebroni.
2 Mambo ya Nyakati 21:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hatimaye Yehoshafati alifariki na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi; naye Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. Biblia Habari Njema - BHND Hatimaye Yehoshafati alifariki na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi; naye Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hatimaye Yehoshafati alifariki na kuzikwa pamoja na babu zake katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi; naye Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. Neno: Bibilia Takatifu Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake. Neno: Maandiko Matakatifu Yehoshafati akalala na baba zake, akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Mwanawe Yehoramu akawa mfalme baada yake. BIBLIA KISWAHILI Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake. |
Nao wakamchukua Asaheli, wakamzika katika kaburi la baba yake, lililokuwako Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakaenda usiku kucha, wakapambazukiwa huko Hebroni.
Basi Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake; na Yehoramu mwanawe akatawala mahali pake.
Akalala Yehoramu na baba zake, akazikwa pamoja na baba zake mjini mwa Daudi; na Ahazia mwanawe akatawala mahali pake.
Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.
Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii juu ya Yehoshafati, akasema, Kwa sababu umepatana na Ahazia, BWANA amezivunjavunja kazi zako. Zikavunjika merikebu, zisiweze kufika Tarshishi.
Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu miaka minane; akafariki bila kutamaniwa; wakamzika mjini mwa Daudi, ila si katika makaburi ya wafalme.
Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Daudi babaye; Rehoboamu mwanawe akatawala badala yake.