Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yoyote utakayowapeleka, wakikuomba, BWANA, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
2 Mambo ya Nyakati 20:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yehoshafati akasimama katikati ya kusanyiko la watu wa Yuda na Yerusalemu mbele ya ua mpya wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Biblia Habari Njema - BHND Yehoshafati akasimama katikati ya kusanyiko la watu wa Yuda na Yerusalemu mbele ya ua mpya wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yehoshafati akasimama katikati ya kusanyiko la watu wa Yuda na Yerusalemu mbele ya ua mpya wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Neno: Bibilia Takatifu Kisha Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, mbele ya ua mpya, Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu la bwana, mbele ya ua mpya, BIBLIA KISWAHILI Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya; |
Ikiwa watu wako watoka kwenda kupigana na adui zao, kwa njia yoyote utakayowapeleka, wakikuomba, BWANA, kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako;
Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA.
akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
Akasimama mfalme mahali pake, akafanya agano mbele za BWANA, kumfuata BWANA, na kuzishika amri zake, na shuhuda zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, kuyatenda maneno ya agano yaliyoandikwa kitabuni humo.
Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako BWANA alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya BWANA, akawaambia watu wote,