Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.
2 Mambo ya Nyakati 20:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wakaja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakakusanyika ili kumwomba Mwenyezi-Mungu awasaidie. Biblia Habari Njema - BHND Watu wakaja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakakusanyika ili kumwomba Mwenyezi-Mungu awasaidie. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wakaja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakakusanyika ili kumwomba Mwenyezi-Mungu awasaidie. Neno: Bibilia Takatifu Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa bwana. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta. BIBLIA KISWAHILI Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA. |
Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao.
Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa BWANA, mbele ya ua mpya;
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.
Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?
Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,