Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi kwa hukumu za BWANA na kesi kati yao. Nao wakarudi Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 19:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akateua waamuzi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliteua waamuzi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, Biblia Habari Njema - BHND Aliteua waamuzi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliteua waamuzi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, Neno: Bibilia Takatifu Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye ngome. Neno: Maandiko Matakatifu Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma. BIBLIA KISWAHILI Akateua waamuzi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; |
Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na wakuu wa jamaa za Waisraeli wawe waamuzi kwa hukumu za BWANA na kesi kati yao. Nao wakarudi Yerusalemu.
Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini hamsini, na wakuu wa kumi kumi;
kisha watatwaa mawe mengine, na kuyatia mahali pa mawe hayo; naye atatwaa chokaa nyingine, na kuipaka chokaa hiyo nyumba.
Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.