Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.
2 Mambo ya Nyakati 17:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu alizitia hofu falme zote jirani na Yuda, zikaogopa kupigana vita na Yehoshafati. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu alizitia hofu falme zote jirani na Yuda, zikaogopa kupigana vita na Yehoshafati. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu alizitia hofu falme zote jirani na Yuda, zikaogopa kupigana vita na Yehoshafati. Neno: Bibilia Takatifu Kicho cha Mwenyezi Mungu kikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati. Neno: Maandiko Matakatifu Hofu ya bwana ikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati. BIBLIA KISWAHILI Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati. |
Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo.
Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; wakawaua Wakushi wengi sana asipone hata mmoja; kwa sababu waliangamizwa mbele za BWANA, na mbele ya jeshi lake; na hao wakachukua mateka wengi sana.
Wakaipiga miji yote kandokando ya Gerari; maana hofu ya BWANA ikawajia; nao wakaiteka nyara miji yote, kwa maana zilikuwamo ndani yake nyara nyingi mno.
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia duniani kote, ili ajionesha kuwa mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa BWANA amepigana juu ya adui za Israeli.
Kwa kuwa mimi nitazitupa nje taifa za watu mbele yako, na kuipanua mipaka yako; wala hapana mtu yeyote atakayeitamani nchi yako, hapo utakapokwea kwenda kuhudhuria mbele za BWANA Mungu wako mara tatu kila mwaka.
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.