Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng'ombe mia saba, na kondoo elfu saba.
2 Mambo ya Nyakati 15:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wote walikusanyika Yerusalemu katika mwezi wa tatu wa mwaka wa kumi na tano wa utawala wake Asa. Biblia Habari Njema - BHND Wote walikusanyika Yerusalemu katika mwezi wa tatu wa mwaka wa kumi na tano wa utawala wake Asa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wote walikusanyika Yerusalemu katika mwezi wa tatu wa mwaka wa kumi na tano wa utawala wake Asa. Neno: Bibilia Takatifu Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. Neno: Maandiko Matakatifu Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. BIBLIA KISWAHILI Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. |
Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng'ombe mia saba, na kondoo elfu saba.
Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimjia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na wakuu wa tarafa na wakuu wa mikoa kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi, mikoa mia moja na ishirini na saba, kila mkoa kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.