Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

2 Mambo ya Nyakati 14:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda elfu mia tatu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, elfu mia mbili na themanini; hao wote walikuwa mashujaa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Mfalme Asa alikuwa na jeshi la askari 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao na mikuki, na wengine 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao na pinde. Wote walikuwa watu mashujaa sana.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Mfalme Asa alikuwa na jeshi la askari 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao na mikuki, na wengine 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao na pinde. Wote walikuwa watu mashujaa sana.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Mfalme Asa alikuwa na jeshi la askari 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao na mikuki, na wengine 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao na pinde. Wote walikuwa watu mashujaa sana.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Asa alikuwa na jeshi la watu elfu mia tatu kutoka Yuda, wenye ngao kubwa na mikuki, na jeshi la watu elfu mia mbili na themanini kutoka Benyamini, wenye ngao ndogo na pinde. Watu hawa wote walikuwa wapiganaji hodari.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Asa alikuwa na jeshi la watu 300,000 kutoka Yuda, wenye ngao kubwa na mikuki na jeshi la watu 280,000 kutoka Benyamini, wenye ngao ndogo na pinde. Watu hawa wote walikuwa wapiganaji mashujaa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda elfu mia tatu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, elfu mia mbili na themanini; hao wote walikuwa mashujaa.

Tazama sura
Tafsiri zingine

2 Mambo ya Nyakati 14:8
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme Sulemani akafanya ngao mia mbili za dhahabu iliyofuliwa; kila ngao moja ilipata shekeli mia sita za dhahabu.

Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia moja na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.

Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule elfu mia moja na themanini waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme.

Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi BWANA;

akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.

Abiya akapanga vita akiwa na jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule elfu mia nne; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake akiwa na watu wateule elfu mia nane, waliokuwa wanaume mashujaa.

Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea BWANA, aliwatia mkononi mwako.

Baada ya hayo, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani.

Tena Amazia akawakusanya Yuda, akawaweka kulingana na nyumba za baba zao chini ya makamanda wa maelfu, na makamanda wa mamia, naam, Yuda pia, na Benyamini; tangu wenye miaka ishirini na zaidi akawahesabu, akawaona kuwa watu wateule elfu mia tatu, wawezao kwenda vitani, waliozoea mkuki na ngao.