Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.
2 Mambo ya Nyakati 13:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa BWANA mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Sasa nyinyi mnadhani mnaweza kupinga ufalme wa Mwenyezi-Mungu aliopewa Daudi na uzao wake kwa sababu eti mnalo jeshi kubwa na sanamu za dhahabu za ndama, alizowatengenezea Yeroboamu kuwa miungu yenu! Biblia Habari Njema - BHND “Sasa nyinyi mnadhani mnaweza kupinga ufalme wa Mwenyezi-Mungu aliopewa Daudi na uzao wake kwa sababu eti mnalo jeshi kubwa na sanamu za dhahabu za ndama, alizowatengenezea Yeroboamu kuwa miungu yenu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Sasa nyinyi mnadhani mnaweza kupinga ufalme wa Mwenyezi-Mungu aliopewa Daudi na uzao wake kwa sababu eti mnalo jeshi kubwa na sanamu za dhahabu za ndama, alizowatengenezea Yeroboamu kuwa miungu yenu! Neno: Bibilia Takatifu “Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa Mwenyezi Mungu ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. Neno: Maandiko Matakatifu “Hata sasa unapanga kupingana na ufalme wa bwana ambao uko mikononi mwa wazao wa Daudi. Kweli ninyi ni jeshi kubwa nanyi mnazo ndama za dhahabu Yeroboamu alizozitengeneza kuwa miungu yenu. BIBLIA KISWAHILI Hata sasa mwajidhania kuwa mtauzuia ufalme wa BWANA mikononi mwa wana wa Daudi; nanyi mmekuwa jamii kubwa, na kwenu mna ndama za dhahabu alizowafanyia Yeroboamu kuwa miungu. |
Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akatengeneza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.
lakini umekosa kuliko wote waliokutangulia, umekwenda kujifanyia miungu mingine, na sanamu zilizoyeyuka, unikasirishe, na kunitupa nyuma yako;
naye akajiwekea makuhani wa mahali pa juu, na wa wale majini, na wa zile ndama alizozitengeneza.
Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.
akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, aliyependezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti chake cha enzi, kuwa mfalme wake BWANA, Mungu wako; kwa kuwa Mungu wako amewapenda Israeli, kuwathibitisha milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme juu yao, ufanye hukumu na haki.
Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.