Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
2 Mambo ya Nyakati 13:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Abiya akapanga vita akiwa na jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule elfu mia nne; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake akiwa na watu wateule elfu mia nane, waliokuwa wanaume mashujaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000. Biblia Habari Njema - BHND Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abiya alijiandaa kupigana vita akiwa na jeshi la askari hodari 400,000, naye Yeroboamu akamkabili na jeshi lake la askari hodari 800,000. Neno: Bibilia Takatifu Abiya aliingia vitani na jeshi la watu elfu mia nne wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu elfu mia nane wenye uwezo. Neno: Maandiko Matakatifu Abiya aliingia vitani na jeshi la watu 400,000 wenye uwezo wa kupigana, naye Yeroboamu akapanga jeshi dhidi ya Abiya akiwa na jeshi la watu 800,000 wenye uwezo. BIBLIA KISWAHILI Abiya akapanga vita akiwa na jeshi la watu hodari wa vita, watu wateule elfu mia nne; naye Yeroboamu akapanga vita juu yake akiwa na watu wateule elfu mia nane, waliokuwa wanaume mashujaa. |
Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu milioni moja na laki moja, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu elfu mia nne sabini (470,000), wenye kufuta panga.
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule elfu mia moja na themanini waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme.
Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka binti Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
Basi Abiya akasimama juu ya kilima cha Semaraimu, kilichoko milimani mwa Efraimu, akasema, Nisikieni, enyi Yeroboamu na Israeli wote;