Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, na mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
2 Mambo ya Nyakati 11:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao. Biblia Habari Njema - BHND Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wote ambao walikuwa wamenuia kwa moyo wa dhati kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kutoka katika makabila yote ya Israeli, waliandamana na Walawi hadi Yerusalemu ili wapate kumtolea tambiko Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao. Neno: Bibilia Takatifu Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea Mwenyezi Mungu dhabihu, Mungu wa baba zao. Neno: Maandiko Matakatifu Wale waliotoka katika kila kabila la Israeli ambao walielekeza mioyo yao kumtafuta bwana, Mungu wa Israeli, wakawafuata Walawi huko Yerusalemu kumtolea bwana dhabihu, Mungu wa baba zao. BIBLIA KISWAHILI Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu BWANA, Mungu wa baba zao. |
Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, na mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya BWANA Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.
Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.
Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.
Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta BWANA, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote;
Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote.
Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimjia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Walakini, yameonekana kiasi cha mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa Maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.
Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza watu wote kufunga katika Yuda yote.
Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute BWANA; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta BWANA.
Ila watu wengine wa Asheri, na wa Manase, na wa Zabuloni walijinyenyekeza, wakaja Yerusalemu.
Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang'anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
na yeye asiyelitia moyoni neno la BWANA akawaacha watumishi wake na wanyama wake mashambani.
Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za BWANA, na kumtafuta BWANA wa majeshi; Mimi nami nitakwenda.
Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.
wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.
akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.
Basi ikiwa hiyo inchi yenu ni najisi, vukeni na kuingia katika nchi ya milki yake BWANA, ambamo maskani ya BWANA inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi BWANA, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya BWANA, Mungu wetu.