Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
2 Mambo ya Nyakati 10:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana wa rika yake, waliokuwa washauri wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini Rehoboamu alipuuza shauri la wazee na badala yake akashauriana na vijana wa rika lake ambao walikuwa washauri wake. Biblia Habari Njema - BHND Lakini Rehoboamu alipuuza shauri la wazee na badala yake akashauriana na vijana wa rika lake ambao walikuwa washauri wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini Rehoboamu alipuuza shauri la wazee na badala yake akashauriana na vijana wa rika lake ambao walikuwa washauri wake. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Rehoboamu akakataa ushauri aliopewa na wazee, na akataka ushauri kwa vijana wa rika lake waliokuwa wakimtumikia. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia. BIBLIA KISWAHILI Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana wa rika yake, waliokuwa washauri wake. |
Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.
Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, kongwa alilotutwika baba yako utufanyie liwe jepesi.
Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.
Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;