Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




2 Mambo ya Nyakati 10:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Naye mfalme Rehoboamu akawajibu kwa ukali, akapuuza shauri la wazee,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Naye mfalme Rehoboamu akawajibu kwa ukali, akapuuza shauri la wazee,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Naye mfalme Rehoboamu akawajibu kwa ukali, akapuuza shauri la wazee,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Alikataa ushauri aliopewa na wazee,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana,

Tazama sura
Tafsiri zingine



2 Mambo ya Nyakati 10:13
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu yule aliye bwana wa nchi alisema nasi kwa maneno makali, akatufanya tu wapelelezi wa nchi.


Yusufu akawaona nduguze, akawatambua, lakini alijifanya kama mgeni kwao. Akasema nao kwa maneno makali, akawaambia, Mmetoka wapi ninyi? Wakasema. Tumetoka nchi ya Kanaani, ili tununue chakula.


Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu.


akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.


Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana wa rika yake, waliokuwa washauri wake.


Farao akamwambia Musa, Nenda zako, ujiangalie, usinione uso tena; kwani siku hiyo utakayoniangalia uso wangu utakufa.


Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.


Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.


Mwanangu, acha kusikia mafundisho, Ukitaka tu kuyaasi maneno ya maarifa.