Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
2 Mambo ya Nyakati 1:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo. Biblia Habari Njema - BHND Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Solomoni alipanda mbele ya madhabahu ya shaba iliyokuwa kwenye hema la mkutano. Hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, akatoa tambiko 1,000 za kuteketezwa juu ya madhabahu hayo. Neno: Bibilia Takatifu Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu elfu moja za sadaka za kuteketezwa juu yake. Neno: Maandiko Matakatifu Sulemani akapanda huko yalikokuwa madhabahu ya shaba mbele za bwana katika Hema la Kukutania, na kutoa dhabihu 1,000 za sadaka za kuteketezwa juu yake. BIBLIA KISWAHILI Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu yake. |
Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu moja za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
Mfalme Sulemani, na mkutano wote wa Israeli waliokutanika kwake, walikuwako pamoja naye mbele ya sanduku, wakichinja sadaka kondoo na ng'ombe, wasioweza kuhesabiwa wala idadi yao kujulikana kwa kuwa wengi.
Sulemani akatoa sadaka za amani, alizomtolea BWANA, ng'ombe elfu ishirini na mbili, na kondoo elfu mia moja na ishirini. Ndivyo mfalme na wana wa Israeli wote walivyoiweka wakfu nyumba ya BWANA.
Siku ya pili yake, wakamtolea BWANA dhabihu, wakamchinjia BWANA sadaka ya kuteketezwa, yaani, ng'ombe elfu moja, na kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji, na dhabihu nyingi kwa ajili ya Israeli wote;
Ndipo Sulemani akamtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA, aliyoijenga mbele ya ukumbi,