Tena gari huja kutoka katika Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia moja na hamsini; hivyo basi watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
2 Mambo ya Nyakati 1:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao walipandisha na kununua gari kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha; na farasi kwa mia moja na hamsini, vivyo hivyo wakawauzia wafalme wote Wahiti na wafalme wa Shamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari. Biblia Habari Njema - BHND Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walinunua gari moja la farasi kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150 za fedha. Kisha waliwauzia wafalme wa Wahiti na Shamu farasi hao na magari. Neno: Bibilia Takatifu Waliagiza magari ya vita kutoka Misri kwa bei ya shekeli mia sita za fedha, na farasi kwa shekeli mia moja na hamsini. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu. Neno: Maandiko Matakatifu Waliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha, na farasi kwa shekeli 150. Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu. BIBLIA KISWAHILI Nao walipandisha na kununua gari kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha; na farasi kwa mia moja na hamsini, vivyo hivyo wakawauzia wafalme wote Wahiti na wafalme wa Shamu. |
Tena gari huja kutoka katika Misri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa mia moja na hamsini; hivyo basi watu wakawaletea wafalme wote wa Wahiti, na wafalme wa Shamu, mikononi mwao.
Walakini katika makosa yake Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, Yehu hakutoka katika kuyafuata, yaani, ndama za dhahabu zilizokuwako katika Betheli na Dani.
Nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi; kila kundi na thamani yake.
Basi Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, na kuujengea ufalme wake nyumba.