Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
1 Yohana 4:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sisi tunapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. Biblia Habari Njema - BHND Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sisi tuna upendo kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. Neno: Bibilia Takatifu Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. Neno: Maandiko Matakatifu Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. BIBLIA KISWAHILI Sisi tunapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. |
Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lolote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.