1 Yohana 3:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo. Biblia Habari Njema - BHND Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wangu, upendo wetu usiwe maneno matupu, bali uwe upendo wa kweli na wa vitendo. Neno: Bibilia Takatifu Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli. BIBLIA KISWAHILI Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. |
Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na subira yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu.
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuayo ile kweli;