Yeye huwatendea ukatili makinda yake, kama kwamba si yake; Ijapokuwa kazi yake yaweza kuwa ya bure, yeye hana hofu;
1 Wathesalonike 2:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndugu, nyinyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure. Biblia Habari Njema - BHND Ndugu, nyinyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndugu, nyinyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure. Neno: Bibilia Takatifu Ndugu zangu, kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua kwamba kuja kwetu kwenu hakukuwa bure, Neno: Maandiko Matakatifu Ndugu zangu, kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ya kwamba kuja kwetu kwenu hakukuwa bure, BIBLIA KISWAHILI Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure; |
Yeye huwatendea ukatili makinda yake, kama kwamba si yake; Ijapokuwa kazi yake yaweza kuwa ya bure, yeye hana hofu;
BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
Lakini nikasema, Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu.
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.
Angalieni; je! Jambo hili halikutoka kwa BWANA wa majeshi, kwamba watu wajishughulikie moto, na mataifa wajisumbue kwa ajili ya ubatili?
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nilizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiria isipokuwa mliamini bure.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Nami nilikwenda kwa kuwa nilifunuliwa, nikawaeleza Injili ile niihubiriyo katika Mataifa, lakini kwa faragha kwa hao viongozi waliosifika, isiwe labda napiga mbio bure, au nilipiga mbio bure.
mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.
Kwa sababu hiyo sisi nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe wa Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na kwa kweli ndivyo lilivyo; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;