Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni.
1 Wakorintho 9:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutofanya kazi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi? Biblia Habari Njema - BHND Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi? Neno: Bibilia Takatifu Au ni mimi na Barnaba tu inatubidi kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu? Neno: Maandiko Matakatifu Au ni mimi na Barnaba tu inatubidi kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu? BIBLIA KISWAHILI Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutofanya kazi? |
Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni.
tena wazaliwa wa kwanza wa wana wetu, na wa wanyama wetu, kama ilivyoandikwa katika torati, na wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe wetu na kondoo wetu, ili kuwaleta nyumbani mwa Mungu wetu, kwa makuhani watumikao nyumbani mwa Mungu wetu;
Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hadi Antiokia.
Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
na kwa kuwa kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi pamoja, kwa maana walikuwa mafundi wa kushona hema.
Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro,
Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.