1 Wakorintho 6:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu yake mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini. Biblia Habari Njema - BHND Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu yake mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpeleka ndugu yake mahakamani, tena mbele ya mahakimu wasioamini. Neno: Bibilia Takatifu Badala yake ndugu mmoja anampeleka mwenzake mahakamani, tena mbele ya watu wasioamini! Neno: Maandiko Matakatifu Badala yake ndugu mmoja anampeleka mwenzake mahakamani, tena mbele ya watu wasioamini! BIBLIA KISWAHILI Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini. |
Kesho yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana?
Je! Mmoja wenu akiwa ana shtaka juu ya mwenzake athubutuje kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu?
Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang'anywa mali zenu?
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.