1 Wakorintho 4:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole? Biblia Habari Njema - BHND Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole? Neno: Bibilia Takatifu Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole? Neno: Maandiko Matakatifu Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole? BIBLIA KISWAHILI Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole? |
kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.
Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;
Nilimwonya Tito, nikamtuma ndugu yule pamoja naye. Je! Tito aliwatoza kitu? Je! Hatukuenenda kwa Roho yeye yule na katika nyayo zile zile?
Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia;
Nami niliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.
Ndugu zangu, mtu akishikwa katika kosa lolote, ninyi mlio wa Roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.