Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
1 Wakorintho 4:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa Ufalme wa Mwenyezi Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. BIBLIA KISWAHILI Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu. |
Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Mgiriki pia.
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kandokando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu;
bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wagiriki, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,
Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika;
ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.