bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,
1 Wakorintho 4:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu wajivunao, bali nguvu zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya. Biblia Habari Njema - BHND Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya. Neno: Bibilia Takatifu Lakini kama Bwana Isa akipenda, nitafika kwenu hivi karibuni, nami nitajua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia nguvu yao. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini kama Bwana Isa akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia kujua nguvu yao. BIBLIA KISWAHILI Lakini nitakuja kwenu upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao tu wajivunao, bali nguvu zao. |
bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,
Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paulo akaazimu rohoni mwake, akiisha kupita katika Makedonia na Akaya, aende Yerusalemu, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi pia.
mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.
Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kutoa unabii, maana yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.
Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia.
Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu natarajia kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia.
Lakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika;
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Lakini mimi namwita Mungu awe shahidi juu ya roho yangu, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho.