Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
1 Wakorintho 3:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; Neno: Bibilia Takatifu Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kama kile alichojenga kitabaki, atapokea thawabu yake. BIBLIA KISWAHILI Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. |
Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe kulingana na taabu yake mwenyewe.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili.
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.
Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji la kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;